Massamba (2011:2) anasema “Nadharia
yoyote mpya hujaribu kuboresha hiyo ya zamani”, Hakuna nadharia mpya inayozuka katika ombe tu.
Kwa mtazamo huo, nadharia mpya
huzaliwa kwa sababu za kuutafiti, kujaribu dhana na kutokea kwa matukio kadhaa
katika maisha. Insha hii itajikita kwa ufupi katika kupitia nadharia za wanamuundo(wanatakisonomia),wanafonolojia
zalishi na nadharia ya wanafonolojia vipande sauti huru ili kujua sababu zilizopelekea kuanzishwa kwa
nadharia ya fonolojia.
Nadharia ya wanataksonomia hawa ni wanafonolojia wa mwanzoni Miongoni mwa waasisi wa nadharia hii ni pamoja
Jan Baudeuin de Courtenay(1845-1929), Ferdinand de Saussure (1857-193), Prince
Nikolaj Sergeevic Trubetzkoy(1890-1939), Daniel Jones (1881-19670, Edward Sapir
91884-1939) na Leonard Bloomfield (1887-1949.Ilijishughulisha na kuchunguza
mabadiliko ya miunganiko ya sauti yanayojitokeza katika mofimu
zinapoungana.Kuchunguza mabadiliko ya sauti yenye kazi ya kimofolojia,vile vile
walijaribu kuelezea namna ambavyo maneno ya lugha yanayotamkwa yangeweza kugawanywa katika makundi mawili,(yaliyopo
akilini mwa msemaji na maneno yenyewe yanayo tamkwa),pia kuyagawa na
kuyaainisha maumbo kivipande vipande na warijaribu kutafuta mbinu au utaratibu
katika kuzibaini fonimu za lugha yeyote ya binaadamu.Ingawa uchanganuzi ulikuwa
ukiainisha maumbo mbalimbali ya sauti au mofu zilizokuwa zikihusiana kimaana au
kiamilifu lakini hawakuonesha uhusiano huo baina ya maumbo hayo.Chomky na Halle
wakaona ni vipi tunaweza kuyahusisha maumbo hayo ndipo nadharia ya kiunzi
rasmi cha fonolojia zalishi ikatokea ili kupunguza tatizo hilo.
Waasisi wa nadharia hii ni Noam
Chomsky na Morris Halle. Wamefanya
uchanganuzi wa vipengele vya kifonolojia katika kitabu chao. “The Sound Pattern of English” (1968).Kiunzi hiki
kinadharia kimejengwa kwenye misingi mikuu mitatu yaani umbo la ndani ambalo
hujengeka katika akili ya msemaji,umbo la nje huwakilisha maneno tutamkayo
katika vinywa vyetu na sauti zote zitumikazo katika lugha asilia ya binaadamu
hutokana na mifumo ya mkondo hewa ambayo ama inakwenda ndani au inatoka nje.pia
matumizi sahihi ya sheria ni jambo lililotiliwa mkazo na kiunzi rasmi cha
fonolojia zalishi.
Kwa mujibu wa Massamba (2011:108)
anasema Kiunzi cha fonolojia zalishi kinawakilisha vipengele mbalimbali vya
kifonolojia kiulalo unaojulikana kama uwakilishi moza (uwakilishi mkururo)
yaani kila kipengele kichambuliwe kisanjari
na hivyo kuchukulia vipamba sauti kama ni vijenzi vya vitamkwa.
Mkabala wa Chomsky na Halle
ulichanganua vipengele vyote vya fonolojia kimoza. Vipengele.walichukulia vipambasauti vyote
kama mkazo,toni,usilabi ni sahemu ya viambajengo vya kitamkwa
kinachohusiana navyo. Mfano katika neno mẽmã:
M ẽ m ᾶ
+midomo -nyuma
+konsonanti - mviringo
+unazali -juu
+korona +vokali
+nazali
Hii ina maana kuwa irabu ẽ inakuwa na sifa ya unazali kwa sababu
inaambukizwa unazali na konsonanti ya nazali iliyoambatana nayo.
Kama mfano unavyoonesha hapo juu
katika uchanganuzi wa vipengele vya kifonolojia, vipambasauti vinachukuliwa
kuwa ni sehemu ya kitamkwa. Hivyo kusababisha kuwa na irabu ẽ yenye unazali na e isiyo na unazali. Kitu
ambacho si sahihi katika lugha ya Kiswahili.
Kwa msingi huu kama unazali
unachukuliwa kuwa ni sehemu ya kitamkwa e mbona katika maneno mengine haiwi
na unazali? Mfano katika neno pema.
Pia tatizo linakuwepo katika
uwakilishi wa toni kwa lugha zenye toni, toni huwa inahama kutoka kwenye silabi
moja kwenda kwenye silabi nyingine, mfano katika kimakonde
Kimakonde Kiswahili
Anίida
– amekuja
Aniida
kύkaya – amekuja nyumbani
Toni juu inaonekana imehama kutoka
katika irabu i katika silabi ni kwenda kwenye irabu u katika silabi ku. Hivyo kusababisha i katika silabi ni kupoteza sifa ya toni juu. Swali la kujiuliza
kama toni juu ni sifa ya irabu hiyo kwa nini isiendelee kuwa nayo sifa hiyo?
Vilevile uwakilishi wa mkazo katika
lugha imeonekana kuwa ni tatizo, mfano katika tungo mtoto, huwa kwa kawaida
katika lugha ya Kiswahili mkazo huwekwa katika silabi ya pili kutoka mwisho.
Hivyo tunakuwa na:
m
toto
( +mkazo)
Hapa silabi to ina mkazo kwa kuwa
ndio silabi ya pili toka mwisho mwa neno hilo, lakini tunapoongeza neno mbele
ikawa mtoto mzuri mkazo unahama kutoka katika silabi to katika
neno mtoto
kwenda katika silabi zu katika neno mzuri. Sasa tujiulize
kama mkazo ni sifa ya silabi to katika neno mtoto, kwani nini sifa
hiyo ipotee kwenda katika silabi zu? Kwa nini isiendelee kubakia
katika silabi to? Hili ni tatizo.
Pia katika uwakilishaji wa usilabi
katika lugha ya Kiswahili. Neno mti asili yake ni muti,
ambapo neno hilo huchukuliwa kuwa na silabi mbili yaani mu na ti.
Na kilele cha silabi huwa ni irabu. Neno muti hutamkwa mti ambapo irabu u
hudondoshwa ambayo ndiyo kilele cha usilabi katika silabi mu, lakini bado usilabi
unabakia katika konsonanti m. Kama usilabi ni sifa ya irabu u
nayo imedondoshwa, kwani nini usilabi uendelee kubakia katika konsonanti m?
pia inaonekana kuna tatizo.
Kutokana na ukweli kwamba sifa za
toni, usilabi, mkazo na unazali katika lugha inaonesha kutohusiana moja kwa
moja na vitamkwa, kwani kitamkwa fulani kinaweza kudondoshwa lakini sifa hiyo
inahamia katika kitamkwa kingine
Kutokana na matatizo ya uwakilishi wa
vipengele mbalimbali vya kifonolojia katika nadharia ya fonolojia zalishi
wataalamu wengine waliibukia na nadharia yao ili kuweza kurekebisha matatizo hayo.
Goldsmith (1977) alikuja na nadharia ya fonolojia vipande sauti huru ambapo kila kitamkwa kilichukuliwa
katika rusu zinazojitegemea.Pia (1975:176) ameeleza kuwa ni nadharia ambayo
ilianzishwa kwa ajili ya kuondoa tatizo ambalo
lilikuwepo baada ya nadharia ya fonolojia zalishi.
Fonolojia vipandesauti
huru (Autosegmental pholology) ni
mtazamo wa kinadharia katika uchanganuzi wa mfumo wa sauti za lugha asilia ambazo umekitwa katika msingi
kwamba kila kipande sauti (kitamkwa, mkazo, toni) hujitegemea na huwa
katika rusu yake chenyewe (si sehemu ya kingine) Massamba (2009:13).
Vipengele vya kifonolojia
vichanganuliwe kwa kutumia uwakilishi rusu.
Rusu hizo huwakilishwa kwa kutumia
mistari ya uhusiano inayodhibitiwa na sharti la ukubalifu (Goldsmith
1976:27) sharti la ukubalifu lina kanuni
tatu:
- Kila toni ihusishwe na angalau irabu moja
- Kila irabu ihusishwe na angalau toni moja
- Mistari ya uhusiano isikingamane,mfano kutoka kimakonde
* Rusu ya kiinitoni(RVt)
Ku kί mbi
la Rusu ya vitamkwa (RV)
Mistari ya uhusiano (MU)
C J C Rusu ya toni(RT)
Pia kufanya uchanganuzi wa Kupunguza
sheria zinazobadili sifa na kutumia kanuni zinazodondosha au kupangilia upya
vipandesauti kwa kutumia njia ya kurekebisha mistari ya uhusiano.
Kwa kuhitimisha kiunzi cha fonolojia zalishi iliibuka kwa kutokana na udhaifu au uliotokana
na wanataksonomia na fonolojia vipande sauti huru iliibuka kutokana na matatizo
ya fonolojia zalishi ambao waliamini
kuwa vipambasauti ni vijenzi vya vitamkwa.japo kuwa wote wanaongelea umbo la nje na la ndani katika
kuchambua fonimu katika lugha na sheria na utaratibu zisizo badilifu
MAREJELEO
Massamba. D.P.B,( 2012) Misingi ya fonolojia,TATAKI ,Dar es salaam
Massamba .D.P.B. (2010) Phonological
Theory History Studies and development:
Institute of Kiswahili Studies, Dar es Salaam
Massamba (2011) Maendeleo katika nadharia ya fonolojia TATAKI, Dar es Salaam
uuuuuiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii
JibuFutani vyema zaidi sisi kama wanazuoni kufanya tafiti zaidi katika suala zima la kukuza na kukipaumbele kiswahili ili kuleta tija zaidio kwa maendeleo ya taifa letu na kupanua wigo wa ajira kupitia lugha yetu ya kiswahili
JibuFutaAhsante madam
JibuFutaEleza kaa mfano mahususi jinsi makundi makuu ya sauti yanayojitofautiana Kaa mujibu wa NOAM CHOMSKY na Moriss HALLE
JibuFutaEleza kaa mfano mahususi jinsi makundi makuu ya sauti yanayojitofautiana Kaa mujibu wa NOAM CHOMSKY na Moriss HALLE
JibuFutaEleza kaa mfano mahususi jinsi makundi makuu ya sauti yanayojitofautiana Kaa mujibu wa NOAM CHOMSKY na Moriss HALLE
JibuFutaAsante kwa kazi mzuri munayoifanya. Nawaomba muendelee hivyo hivyo kwani munatusaidia sana sisi wanafunzi wa isimu katika vyuo vikuu
JibuFuta